Jumla ya Waganga wa Tiba Asili 16 wa Wilaya ya Mwanga, leo tar 12.09.2018 wamekabidhiwa vyeti vya usajili ambavyo vinawatambua rasmi kama sehemu ya Waganga wa tiba asili waliosajiliwa hapa Wilayani Mwanga.
Zoezi hilo la kukabidhi vyeti limefanywa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bwana Aaron Yesaya Mbogho. Akiwa anakabidhi vyeti hivyo, Mhe. Mkuu wa Wilaya amewasisitiza waganga hao kuhakikisha kuwa wanafanya kazi zao za uganga kwa maadili mazuri pasipo kuvunja sheria za nchi. Pia Mkuu wa Wilaya amewasisitiza viongozi wa Chama cha Tiba Asili wa Wilaya ya Mwanga kuhakikisha kuwa, wanawahamasisha waganga wengine wa tiba asilia ambao hawajasajiliwa ili waweze kusajiliwa na waweze kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Dr. Taramael W. Ndosi amewaelekeza Waganga hao kuhakikisha kuwa hawapigi ramli, watunze mazingira, wasajili vifaa vya maliasili, wasajili madawa na mitishamba yao, watunze mazingira na mwisho kila mganga wa tiba asilia ahakikishe amesajiliwa na kupata leseni kisheria.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa