Kamati ya ALAT ya Mkoa wa Kilimanjaro leo imezuru Wilaya ya Mwanga ikiongozwa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Ndg. Salehe R. Mkwizu kwa lengo la kutembelea na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Halmasahuri ya Wilaya ya Mwanga.
Katika ziara yake hiyo, kamati imefanikiwa kutembelea miradi minne ambayo ni mradi wa kimkakati wa Halmashauri ya Mwanga wa Kufyatua matofali, shule ya Sekondari Ngolea, mradi wa ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Lang’ata Bora na mradi wa chakula barafu unao jumuisha ujenzi wa vizimba 24 vya kuuzia samaki.
Miradi hii ambayo ina thamani ya Tsh. Milioni 172,324,700/= kwa asilimia kubwa imejengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi ambao wamechangia michango pamoja na nguvu kazi zao.
Wajumbe hao wa ALAT watakuwa na ziara ya siku mbili Wilayani Mwanga ambapo siku ya tarehe 18 Machi, 2022 watakaa na kufanya majumuisho ya ziara hiyo na baadae wataendelea na ziara kwenye wilaya zingine za Moa wa Kilimanjaro.
ALAT ni Jumuiya ya Tawala za Mikoa Tanzania ambayo majukumu ya msingi ya Jumuiya hii ni pamoja na usimamizi, uwakilishi, utetezi, ushawishi na utoaji huduma katika serikali za mitaa. Jumuiya huziwakilisha Serikali za Mitaa katika mikutano ya kitaifa na kimataifa inayohusu Serikali za Mitaa. Jumuia hii pia huwasilisha Serikalini maoni na mapendekezo ya Serikali za Mitaa kuhusu jambo lolote ambalo linaonekana ni la manufaa kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa