Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Ndg. Aaron Y. Mbogho, jana amezindua rasmi zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya Taifa katika Wilaya ya Mwanga ambapo jumla ya vitambulisho 24,457 viko tayari.
Akiwa anasoma taarifa ya zoezi la uandikishaji mbele ya Mkuu wa Wilaya, Afisa Msajili wa Vitambulisho Wilaya, Ndg. Sebastian Rwegerela alisema, katika zoezi la kusajili/kuandikisha, wamefanikiwa kuandikisha wananchi 50,325 kati ya 50,955 ambapo ni sawa na asilimia 98.76. Alisema kuwa mpaka sasa ofisi yake imesha andaa vitambulisho 24,457 tayari kwaajili ya kuvigawa kwa wahusika na vitambulisho vingine ambavyo bado watavigawa kwa wakati mara vitakapokuwa tayari. Aliendelea kusema kuwa, mpaka sasa kuna jumla ya wananchi 630 ambao bado hawajasajiliwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wengine kusafiri, kuwa shuleni na wengine ni wafanya biashara wanaotoka mara kwa mara. Alisema, wananchi ambao hawajasajiliwa, wataendelea kupatiwa huduma ya usajili ndani ya ofisi za NIDA Wilaya.
Pamoja na mafanikio hayo ya uandikishaji, Ndg. Sebastian alieleza kuwa, kuna changamoto chache ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ambazo ni baadhi ya wananchi kutotaka kujiandikisha na kutokuwepo kwa ofisi ya Uhamiaji Wilaya japo kwa sasa ofisi ipo mbioni kufunguliwa.
Aidha, ofisi ya NIDA Wilaya, imetoa shukrani nyingi kwa wadau mbalimbali waliohusika na wanaoendelea kutoa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa, zoezi la uandikishaji linafanikiwa vizuri.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa