Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda mapema leo amefanya ziara ya kikazi Wilayani Mwanga ambapo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kilaweni.
Katika ziara hiyo wananchi wa Mwanga wakiwakilishwa na mbunge wao Mhe. Joseph Anania Thadayo wamemwomba mhe waziri kwa mamlaka aliyonayo aifanye shule hiyo iwe moja ya shule ya amali.
Baada kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo Mhe. Waziri ameridhia ombi hilo na kuagiza wataalamu kutoka VETA kuanza kwa haraka mchakato wa mapitio ya mradi ili kuharakisha utekelezaji huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa