Hayo yamesemwa leo na Afisa Lishe wa Wilaya ya Mwanga, Ndg. Jacob Minja alipokuwa akiwasilisha taarifa fupi ya utoaji wa matone ya vitamin ''A'' kwa wajumbe wa kamati ya lishe Wilaya.
Ndg. Minja amesema kuwa, vitamin hiyo pamoja na dawa hutolewa kila ifikapo mwezi juni na desemba ya kila mwaka na kwa mwaka jana kwa mwezi juni walengwa walikuwa watoto 18,495 ambapo waliopata ni watoto 18,115 sawa na 98%, na waliopata dawa za minyoo ni watoto 15,591 kati ya watoto 16,110 ya walengwa, sawa na 97%.
Serikali kwa asilimia kubwa, imekuwa ikisimamia suala la lishe kwa jamii husani kwa watoto ili kuhakikisha kuwa, wanakuwa na lishe nzuri na ya kuridhisha.
Kama inavyofahamika, upungufu wa vitamin "A" ndio chanzo kikuu cha upofu wa macho kwa watoto ambao unazuilika kwa urahisi. Uwepo wa vitamin "A" mwilini husaidia mwili kujikinga na maradhi mbalimbali hasa Surua, magonjwa ya mfumo wa hewa na kuharisha.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa