Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga ambayo ni miongoni mwa Halmashauri saba za Mkoa wa Kilimanjaro, imekuwa ikifanya vizuri katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa.
Michezo hiyo ambayo inajumuisha michezo mbalimbali, ilianza jana katika viwanja vya shule ya Sekondari Moshi Ufundi. Wilaya ya Mwanga imekuwa tishio katika michezo hiyo haswa katika mchezo wa soka wavulana ambapo, jana ilifanikiwa kuifunga timu ya Halmashauri ya Rombo mabao 2-0, leo pia wameweza kuifunga Halmashauri ya Same mabao 3-0, huku wakiifunga Halmashauri ya Wilaya ya Siha bao 1-0. Katika ushindi huu, Halmashauri ya Mwanga imeshatinga hatua ya nusu fainali kwa kujikusanyia jumla ya alama 9 na magoli 6.
Aidha katika mchezo wa soka maalum, Halmashauri ya Mwanga wameifungu Manispaa ya Moshi jumla ya mabao 6-1. Katika mchezo wa netiboli, Halmashauri ya Mwanga imewafunga Halmashauri ya Same mabao 21-19, pia wakawafunga Halmashauri ya Hai magoli 20-15, huku katika mchezo wa kikapu (Wasichana), Halmashauri ya Mwanga ikiwafunga Halmashauri ya Same kwa jumla ya vikapu 14-10.
Michezo hiyo itaendelea tena siku ya kesho na inategemea kuhitimishwa tarehe 20 Mei, 2023 ambapo timu ya Mkoa itakuwa imeundwa, na kuanza kukaa kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Taifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa