Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, Ndg. Zefrin K. Lubuva, amewapongeza watumishi wa Halmashauri yake kwa kuweza kutimiza adhma ya Serikali kwa kuvitangaza vivutio vya ndani vya utalii.
Mkurugenzi mtendaji aliyazungumza hayo tarehe 04.11.2019wakati alipojumuika na watumishi wake kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliyopo Mkoani Arusha. Alisema kuwa, watumishi wamefanya kitu kizuri kwani, ilani ya Serikali ilyopo madarakani imetamka wazi kuwa, utalii lazima ukuwe kwa kupitia njia mbalimbali, ikiwemo kuutangaza kupitia taasisi za umma. Aliendelea kusema kuwa, Halmashauri ya Mwanga, kwa kupitia watumishi wake wametekeleza kwa vitendo ilani ya ya Serikali kwa kuutangaza utalii.
Nao watumishi waliosafiri katika safari hiyo hawakuacha kuelezea furaha yao katika safari hiyo. Wakiongea kwa nyakati tofauti walisema, tumefurahi sana kutembelea moja wapo ya vivutio maarufu hapa Tanzania na tunamshukuru sana Mkurugenzi wetu kwa kuungana na sisi na pia tunamshukuru kwa kutupa kibali cha kuja katika hifadhi ya Ngorongoro, aliongea mmojawapo wa watumishi.
Hata hivyo watumishi hawakuacha kuweka wazi dhamira yao ya kuendelea na moyo wa kuvitangaza vivutio vya kitalii vya nchi kwa kusema, wakati mwingine watatembelea vivutio vya sehemu zingine zenye vivutio vya kitalii ili kuendelea kuutangaza utalii wa nchi.
Serikali imekuwa ikiwahimiza sana wananchi kutembelea vivutio vya kitalii vilivyoko hapa nchini. Na kwa kulizingatia hilo, Serikali imeweka gharama za chini kwa wazawa wanaotaka kutembelea maeneo hayo.
Hata hivyo, inatakiwa watanzania tuendelee kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vyetu kwani Serikali imeweka jitihada za makusudi za kuhakikisha vivutio hivyo, vinalindwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadae.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa