Ikiwa ni mpango wa Serikali kudhibiti vitendo vya kikatili na vya unyanyasaji dhidi ya wanawake na watoto, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga kwa kushirikiana na asasi zisizokuwa za Serikali, imefanikiwa kuunda na kutoa mafunzo kwa kamati maalum itakayo kuwa ikifuatilia, kutoa elimu, kuibua vitendo vya kikatili na kusimamia haki ya wanawake na watoto hapa Wilayani.
Mafunzo hayo ambayo yametolewa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, yamewajengea uwezo wanakamati, namna ya kuweza kukabiliana na vitendo vya kikatili dhidi ya wanaweka na watoto. Vitendo vya kikatili dhidi ya watoto ni pamoja na kunyimwa haki ya elimu, kuishi, kulindwa, chakula, elimu, huduma za afya, ulinzi, kuishi na wazazi, kucheza nk. Vitendo vya mikatili dhidi ya wanawake ni pamoja na ukeketaji, kutorithishwa mali, ndoa za utotoni, mimba za utotoni, kutopatiwa elimu nk.
Kamati hii ina jukumu kubwa la kuhakikisha inapambana na vitendo vyote vinavyo mnyanyasa mwanamke na watoto ili kuweza kuleta usawa na maendeleo katika jamii. Kwa kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kutapelekea Taifa kuwa na vizazi vyenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya uchumi, jamii, siasa na elimu, hii ikiwa ni sehemu ya mpango na mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa inafikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa