Zoezi la uzinduzi wa mpango wa TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, kipindi cha pili cha awamu ya tatu limefanyika leo. Zoezi hili limezinduliwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Ndg. Abdallah Mwaipaya.
Mhe. Mkuu wa Wilaya katika hotuba yake amesema, ana imani kuwa viongozi na watendaji walioshiriki katika uzinduzi huo watazingatia maelekezo yote yatakayokuwa yametolewa. "Nawasisitiza watendaji kuwa waadilifu tunapoanza utekelezaji wa mpango, tukafanye kazi kwa uadilifu ili tufikie malengo ya Serikali" alisema Mkuu wa Wilaya. Ameendelea kusema kuwa, awamu ya tatu ya TASAF imezingatia vyema changamoto ambazo zilijitokeza katika utekelezaji wa kipindi cha kwanza hivyo kuja na maboresho zaidi katika awamu hii.
Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Mwajuma A. Nasombe amesema, jumla ya vijiji 32 katika awamu hii vitanufaika na mpango wa sasa na kufanya jumla ya vijiji vyote 72 vya Wilaya ya Mwanga kuwa sehemu ya mpango wa TASAF. Ametumia pia fursa hiyo kuwahasa watendaji wake kuhakikisha kuwa, walengwa watakaoingizwa kwenye mpango wawe ni watu sahihi na siyo vinginevyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa