Huku Serikali ikihakikisha kuwa inapambana kwa kasi katika kupambana na ugonjwa hatari wa Corona, Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga leo imepokea vifaa vya kisasa kumi kwa ajili ya kunawia mikono. Vifaa hivi vimetolewa na taasisi ya Dr. Msuya Foundation ya Mkoani Fodoma.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa Wilaya ya Mwanga, Ndg. Ombeni Msuya, ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo amesema, mbali na kutoa misaada mbalimbali kwenye jamii ya watanzania, taasisi yake imeona ni vyema pia kutoa msaada kwa tasisi zingine kwa ajili ya kutoa ushirikiano wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona. Mkurugenzi huyu hakuacha kusifia uongozi wa Wilaya kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kupambana na ugonjwa huu. Pia ameendelea kusema, anafurahishwa sana na shughuli za maendeleo zinazofanywa Wilayani Mwanga, ikiwa ni pamoja na utunzaji mzuri wa mazingira.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Ndg. Zefrin K. Lubuva, akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Thomas Apson, alitoa shukrani nyingi kwa taasisi ya Dr. Msuya Foundation kwa mchango wao muhimu kwa Wilaya kwa kuhakikisha kuwa, wanatoa ushirikiano katika kupambana na ugonjwa wa Corona. Ndg. Lubuva amewahakikishia wafadhili hao kuwa, vifaa husika, vitatumika kama ilivyokusudiwa. Aliongeza kwa kusema kuwa, vifaa hivi, vitatawanywa kwenye sehemu zenye mikusanyiko mingi ya watu kama sokoni, hispitali na kwenye taasisi zingine.
Taasisi ya Dr. Msuya Foundation ni taasisi inayojihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali kwenye jamii na kwenye taasisi za umma na taasisi binafsi. Taasisi mpaka sasa wameshatoa ufadhili wa vifaa mbalimbali vya kunawia mikono kwenye taasisi kama misikitini, makanisani na kwenye taasisi za umma.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa