Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga imepata fursa ya kuwa mwenyeji Kimkoa, katika kuadhimisha siku ya Wauguzi Duniani.
Maadhimisho hayo yalianza tarehe 03.05.2019 kwa kutoa huduma ya afya bure katika shule za msingi na sekondari, na leo tarehe 09.05.2019 yamefunguliwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Ndg. Thomas K. Apson na kilele chake itakuwa tarehe 12.05.2019 ambapo mgeni rasmi atakuwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dr. Anna Mghwira.
Akielezea huduma za kiafya ambazo wananchi wa Mwanga watazipata bure, mpaka tarehe 11.05.2019, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Gaudensia Aloyce Olomi alisema, huduma hizo ambazo zitatolewa katika uwanja wa mpira wa C.D Msuya ni pamoja na, uchangiaji damu salama, kupima na kutoa elimu kuhusu maambukizi ya VVU, kutoa elimu na chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi (HPV), uchunguzi wa kifua kikuu, kupima sukari, kupima shinikizo la damu, kupima uzito na urefu, kuchunguza saratani ya matiti pamoja na kutoa elimu ya uzazi.
Siku ya wauguzi ni siku ambayo huwa inafanyika ili kumuenzi muasisi wa huduma za uuguzi Duniani Bi. Florence Nightngale, ambaye alizaliwa mwaka 1820 huko Italia na kufariki mwaka 1910. Muasisi huyo alifanya kazi ya kutoa huduma kwa jamii, hususani waathirika wa vita vya kwanza vya Dunia.
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
Sanduku la Posta: 176 Mwanga,Kilimanjaro
Simu ya Mezani: +255 272974343
Namba ya Simu: +255 272974343
Barua Pepe: ded@mwangadc.go.tz
hatimiliki ©2022 Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga . Haki zote zimehifadhiwa